Gazeti la Al Jamhuriyyah la Lebanon limeandika kuwa, hivi karibuni Harakati
ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ilifanya manuva kubwa ya
kijeshi iliyowashirikisha wapiganaji shupavu wa harakati hiyo wapatao elfu
10.
Gazeti hilo limeendelea kuandika kuwa, manuva hiyo imefanyika kwa minajili ya
kujiweka tayari kwa chokochoko zozote za utawala wa Kizayuni wa Israel na
yalifanyika katika maeneo kadhaa ya kusini na mashariki mwa Lebanon.
Aidha gazeti hilo limeandika kuwa, manuva hayo yalifanyika kwa muda wa siku
tatu. Manuva hayo yaliyowashirikisha vijana wenye umri wa miaka 16 hadi 20
yanahesabiwa kuwa ya kwanza na ya aina yake ambayo yamewahi kufanywa na
Hizbullah katika maeneo yaliyochini ya udhibiti wake.
Pia katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah
ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba utakabiliwa na tsunami ya
makombora yenye nguvu zaidi kuliko Fajr 5 katika miji yote ya Palestina
inayokaliwa kwa mabavu ukiwemo Tel Aviv, iwapo utawala huo khabithi utaanzisha
tena chokochoko dhidi ya ardhi ya Lebanon. Akizungumza na waumini waliokuwa
wakiomboleza Ashura ya Imam Hussein AS kusini mwa Beirut, Sayyid Hassan
Nasrullah amehoji kuwa, utawala wa Israel umetiwa kiwewe na makombora machache
tu ya Fajr 5 yaliyorushwa na wapiganaji wa Hamas wa Kipalestina, vipi utaweza
kustahamili kishindo cha maelfu ya makombora yenye nguvu zaidi ya Hizbullah
yatakayokita kwenye miji yote ya utawala huo? Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongeza
kuwa, utawala wa Israel unaelekea kusambaratika kwani kwa muda mrefu umekuwa
ukiingiwa na kitete mbele ya wanamuqawama.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO