Friday, December 21, 2012

ARAB LEAGUE KUFANYIA MKUTANO WAO PALESTINA



Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu (Arab League) wametoa pendekezo la kufanyika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan huko Palestina.
Afisa mmoja wa Arab League amesema kuwa sekretarieti ya jumuiya hiyo imewasilisha pendekezo la Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas na Katibu Mkuu wa Arab League Nabil Al Arabi la kufanyika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya hiyo Ukingo wa Magharibi kwa nchi zote wanachama. Afisa huyo ameongeza kuwa lengo la kutaka kufanyika mkutano huo huko Ramallah ni kuchunguza hali ya ndani ya Palestina na kutangaza mshikamano wa nchi za Kiarabu na wananchi wa Palestina katika kipindi kigumu cha sasa.
Mawaziri kadhaa wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu walitembelea Ukanda wa Ghaza wakati na baada ya mashambulizi ya siku nane ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO