Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, nguvu kubwa iliyoonyeshwa na wananchi wa Iran, imeweza kuzima njama zote za maadui. Akizungumza kwenye Kongamano la Wakuu wa Mikoa hapa nchini, Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa, katika hali ambayo maadui wamekuwa wakiongeza mbinyo na mzingiro wao siku hadi siku, wananchi wa Iran wameweza kuonyesha nguvu na uwezo wao kwa kuwashinda maadui. Ameongeza kuwa, wananchi wa Iran wamevibadilisha vikwazo vya upande mmoja vya nchi za Magharibi na kuwa fursa ya kupiga hatua za kimaendeleo hapa nchini. Rais Mahmoud Ahmadinejad amebainisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika hapo mwakani na kuongeza kuwa, wananchi wa Iran wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo kama ilivyokuwa kwenye chaguzi zilizopita, na kamwe maadui hawawezi kuziathiri irada za wananchi wa Iran. Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa, uchaguzi wa Iran umekuwa ukitoa athari kubwa katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu mzima, kutokana umuhimu maalumu uliokuwa nao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO