Saturday, February 09, 2013

IRAN YAONYESHA KIWANDA CHA KUTENGENEZA DRONE ZAKE


Kwa mara ya kwanza Iran imesambaza taswira za kiwanda chake kinachotengeneza ndege zisizo na rubani yaani Drone zinazoshabihiana kikamilifu na ile drone ya Marekani ya ScanEagle.

Ndege hizo zisizo na rubani zinatengenezwa kikamilifu hapa nchini na sasa zinatumiwa na Vikosi vya Kijeshi vya Iran.
Ikumbukwe kuwa Desemba 4 mwaka 2012 Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilitangaza kuwa lilifanikiwa kunasa ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya ScanEagle katika maji ya Ghuba ya Uajemi. Kamanda wa Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Admeri Ali Fadavi alisema kuwa wataalamu wa jeshi hilo walifanikiwa kushusha chini na kuinasa ndege hiyo isiyo na rubani ya Marekani ambayo ilikuwa imeingia katika anga ya Iran ikiongozwa kutoka mbali.
Hivi karibuni pia Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilionyesha taswira zilizokuwa zimechukuliwa na drone nyingine ya kisasa ya Marekani aina ya RQ-170 iliyonaswa ikifanya ujasusi nchini Iran. Wataalamu wa Iran wamefanikiwa kutanzua habari zote za siri katika ndege hiyo ya kisasa kabisa ya kijasusi. Drone hiyo ilinaswa katika oparesheni maalumu ya vikosi vya Iran katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi mnamo Desemba mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO