Tuesday, December 18, 2012

INTIFADHA YA TATU YAKARIBIA YA WAPALESTINA YAKARIBIA


Gazeti  la Yediot Aharanot la utawala wa Kizayuni wa Israel limeripoti habari ya kukaribia kuanza mapambano ya Intifadha ya Tatu ya Palestina katika mji wa al Khalil ulioko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Gazeti hilo limeandika kuwa, kuendelezwa maandamano ya kila wiki dhidi ya ukuta eti wa usalama, uchokozi wa wanajeshi wa Israel katika baadhi ya miji na vijiji vya eneo hilo na hali kadhalika maandamano yanayofanywa na wananchi wa Palestina wa maeneo ya Ramallah, Tulkaram na Qalqililya katika kuiunga mkono Harakati ya Mapambano ya Palestina Hamas, hayo yote yanaonyesha kukaribia kuanza Intifadha ya Tatu ya wananchi wa Palestina.
Naye Raed Ridhwan Katibu Mkuu wa Harakati  ya Kipalestina ya Fat-h amesema kuwa, kuendelezwa vitendo vya uchokozi na ukandamizaji vya Wazayuni dhidi ya Wapalestina, vitasababisha kuanzishwa intifadha mpya ya Wapalestina.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO