Tuesday, December 18, 2012

ISRAEL YASEMA QUDS MJI MTAKATIFU WA WAPESTINA NI ENEO LAO

Izzat al Rishq, mjumbe mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Quds, ni mji mkuu wa milele wa Palestina na umma wa Kiislamu na Kiarabu. Matamshi ya kiongozi huyo mwandamizi wa HAMAS yamekuja kujibu matamshi makali ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel aliyejigamba kuwa Quds, milele itakuwa ni mali ya Israel. Wapalestina wanasema kuwa, matamshi ya Netanyahu ya kwamba mji wa Quds ulikuwa mali ya Mayahudi tangu miaka elfu tatu iliyopita ni njama tu za kuwafanyia ghilba walowezi wa Kizayuni na kuhalilisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi hao katika ardhi walizoporwa Wapalestina. Lakini Wapalestina wanasema kuwa madai kama hayo kamwe hayawezi kubatilisha ukweli wa kihistoria na kijiografia wa mji wa Baytul Muqaddas. 

Weledi wa mambo wanaamini kuwa, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amepoteza umashuhuri wake wa kisiasa baada ya Israel kushindwa vibaya katika vita vya siku 8 vya Ghaza, kiasi kwamba sasa analazimika kukimbilia kwenye kupotosha uhakika wa kihistoria ili kuvutia fikra za Wazayuni wanaopiga kura. Mji wa Quds ni miongoni mwa masuala ambayo yamekuwa yakileta migogoro wakati wote katika kipindi chote hiki cha miongo sita ya kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel. Makuhani wa Kizayuni nao wamekuwa wakipiga propaganda kubwa ili kuzipaka rangi ya dini siasa za kupenda kujitanua za utawala wa Kizayuni. Baytul Muqaddas ni mji mtakatifu wa kihistoria wenye athari nyingi za kitaifa na kidini za Wapalestina. Miongoni mwa vitu vinavyoutambulisha mji huo mtukufu na ambavyo havikanushiki ni majengo yake ya zamani sana ya kidini na kihistoria kama vile misikiti na makanisa ya kale. Kabla ya miaka 60 na kidogo ya kukaliwa kwa mabavu Palestina na walowezi wa Kizayuni kutoka nje, mji huo Palestina kiujumla ilikuwa imo mikononi mwa Waislamu ambao walikuwa wakiishi salama kabisa na wananchi wenzao Wakristo na Mayahudi na hakukuwa na Myahudi wala Mkristo aliyebaguliwa au kunyimwa haki zake.

 Hata hivyo hivi sasa Wazayuni wanafanya njama za kupotosha ukweli wa kihistoria kwa kupiga propaganda kubwa za kuonyesha kuwa mji huo ni mali ya Mayahudi tu, na wasio Mayahudi hawana haki katika mji huo. Utawala wa Kizayuni umekuwa ukivunja misikiti na makanisa pamoja na majengo na maeneo ya kihistoria na kujenga kwa wingi vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ili kubadilisha muundo wa kijiografia na kijamii wa mji huo na wakati huo huo kueneza propaganda kuwa mji huyo ni mali ya milele ya Mayahudi. Hivi sasa utawala wa Kizayuni umeugawa mapande mawili mji wa Quds, yaani Quds Magharibi na Quds Mashariki. Eneo la Quds Magharibi limekuwa likikaliwa kwa mabavu na Wazayuni kwa muda wa miaka 64 sasa yaani tangu mwaka 1948 ulipoundwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Hata hivyo hadi hivi sasa Wazayuni wameshindwa kulikalia kikamilifu eneo la mashariki mwa mji huo mtukufu. Pamoja na hayo lakini, utawala huo umekuwa ukifanya njama nyingi za kuharibu maeneo matakatifu ikiwa ni pamoja na kibla cha kwanza cha Waislamu yaani msikiti wa al Aqsa. Wazayuni ni maadui wa haki na hawamhurumii Muislamu, wala Mkristo na wala Myahudi anayepinga siasa zao za kibeberu, hivyo njia pekee ya kuweza kukabiliana na donda hili ndugu la saratani, ni kuunganishwa pamoja nguvu za wapenda haki wote ulimwenguni katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO