Tuesday, December 18, 2012

MAREKANI SI NCHI YA KUIAMINI


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uzoefu unaonyesha kuwa, matamshi yanayotolewa na viongozi wa Marekani sio ya kuaminika.
Akitoa radiamali yake kuhusiana na matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na viongozi wa Washington kuwa wako tayari kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Iran, Ali Akbar Salehi ameongeza kuwa, mazungumzo yanapaswa kufanyika mazingira sawa na kuonyesha azma ya kweli, lakini kuzidishwa mashinikizo na nyendo za kiadui dhidi ya upande wa pili, hakuna maana yoyote ya kutolewa madai ya kutaka kufanya  mazungumzo ya moja kwa moja. Salehi amesema kuwa, mazungumzo ndiyo njia pekee ya kimsingi ambayo inatumia gharama ndogo katika kutatua matatizo na kusisitiza kuwa, Iran imekuwa ikichunguza kwa makini nyendo za Marekani lakini imegundua kwamba hakuna mabadiliko yoyote kwenye siasa za nchi hiyo zilizo dhidi ya wananchi wa Iran. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, kutumwa ndege za kijasusi za Marekani kwenye anga ya Iran, vikwazo vya upande mmoja vinavyowekwa dhidi ya Iran, kuyasaidia makundi ya kigaidi katika kuwauwa wataalamu wa nyuklia wa Iran, hayo yote hayaonyeshi kwamba Marekani ina nia njema ya kufanya mazungumzo na Iran.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO