Askofu Desmond Tutu mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel amesema kuwa, Umoja wa
Ulaya unashirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kutenda jinai dhidi
ya wananchi wa Palestina. Askofu Tutu ameongeza kuwa, umoja huo unazidi kuongeza
mashirikiano yake na utawala wa Israel, katika hali ambayo wananchi wengi wa
Ulaya kwa hivi sasa wanaitazama Israel kwa mtazamo hasi. Askofu Tutu amesema
Israel ni utawala unaotenda vitendo vya kibaguzi dhidi ya Wapalestina. Kiongozi
huyo wa kidini wa Afrika Kusini ambaye alikuwa na nafasi muhimu katika harakati
za mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini,
amesisitiza kwamba ubaguzi wa Israel ni mbaya zaidi kuliko wa utawala huo wa
zamani wa makaburu
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO