Tuesday, December 25, 2012

MAKANISA YACHOMWA MOTO AUSTRALIA

Makanisa matatu yameteketezwa kwa moto nchini Austria wakati wa kuwadia mkesha wa siku aliyozaliwa Issa Masih AS. Taarifa zinasema kuwa, Makanisa hayo yamechomwa moto na watu wasiojulikana katika mji wa Amstetten ulioko umbali wa kilomita 130 magharibi mwa Vienna mji mkuu wa nchi hiyo. Hadi sasa  Polisi ya Austria haijapata taarifa za kundi au mtu aliyehusika na tukio hilo, amma imeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kimeshaanza kueleweka. 

Mmoja kati ya viongozi wa Kanisa moja lililoteketezwa amesema kuwa, tukio hilo limesababisha hasara ya  mamilioni ya euro. Hali kadhalika amekadhibisha madai kuwa kuchomwa moto Makanisa hayo kumetokana na sababu za kisiasa, ingawa  amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wao kwa kina na kuwatia mbaroni wale wote waliohusika na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO