Tuesday, December 25, 2012

HATIMAYE UN NAO WAYAONA MADHARA WAPATAYO WAISLAM WA MYANMAR


Umoja wa Mataifa umeeleza wasi wasi ulionao kuhusiana na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya huko nchini Myanmar.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio linaloitaka serikali ya Myanmar iheshimu haki za Waislamu wa Rohingya na ichukue hatua za maana kwa ajili ya kuboresha hali ya maisha ya Waislamu hao.
Jana wanachama 193 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walisisitiza katika azimio hilo kwamba, serikali ya Myanmar inapaswa kutambua rasmi uraia wa Waislamu wa Rohingya.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, licha ya kuweko mageuzi ya kisiasa yaliyofanywa na serikali ya Myanmar lakini, nchi hiyo ingali inashuhudia ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu na uhuru wa mtu binafsi.
Waislamu wa jamii ya Rohingya huko Myanmar wanaendelea kutendewa ukatili na Mabudha huku mashirika yanayodai kutetea haki za binaadamu ulimwenguni na madola ya Magharibi yakinyamaza kimya na kujifanya hayasikii kilio cha walimwengu cha kutaka kukomeshwa jinai dhidi ya Waislamu hao.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO