Wataalamu wa kisiasa na masuala ya kijamii katika nchi za Kiarabu wanasema kuwa, kuna ukiukaji mkubwa wa haki za wanawake katika nchi za Kiarabu na hasa nchini Saudi Arabia. Ahmad Juma Mtaalamu wa masuala ya siasa za Kiarabu amesema kuwa, ukatili na ukandamizaji dhidi ya wanawake lipo katika nchi nyingi duniani, amma mushkeli wa wanawake wa Saudi Arabia na baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo la Mashariki ya Kati ni mkubwa, kwani unawanyima uhuru wa kufungua mashtaka, na hata kama idara ya polisi ikikubali kufanywa uchunguzi wa madai yao, hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya wahalifu. Ahmad Juma ameongeza kuwa, wanawake wa Saudia hawana haki ya kutafuta elimu, kurithi na kumiliki mali binafsi, kwani wao wanahesabiwa kuwa ni mali na wala siyo binadamu. Mtaalamu huyo amesema kuwa, viongozi wa Saudi Arabia wanataka kupitisha sheria inayowapiga marufuku wanawake kusafiri, kufanya kazi na kujishughulisha shughuli za kisiasa. Hivi karibuni, Adila bint Abdullah al Saud Mkuu wa Mpango wa Usalama wa Familia katika jimbo la Najran kusini mwa Saudi Arabia amesema kuwa, ukandamizaji na ukatili wa kifamilia, ndio sababu kuu ya vifo vya wanawake wa Saudi Arabia. Ameongeza kuwa, takwimu ya vifo vya wanawake na wasichana wa Saudi Arabia vinavyotokana na vitendo vya ukatili na ukandamizaji dhidi yao, ni kubwa mno kuliko vifo vya wanawake vinavyosababishwa na maradhi na ajali za barabarani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO