Sunday, December 23, 2012

MAREKANI YAPELEKA MANOWARI MBILI IRAQ

Marekani imewasilisha manowari mbili za kutoa usaidizi wa kijeshi kwa Iraq, ambayo inalenga kuimarisha uwezo wake wa doria za majini. Taarifa ya ubalozi wa Marekani imesema meli hizo mbili zenye urefu wa mita 60 kila moja zimewasilishwa na jeshi la maji la Marekani mnamo tarehe 20 mwezi huu. Meli hizo zinaweza kutumiwa kwa majukumu mengi ikiwa ni pamoja na kuzisaidia operesheni za jeshi la majini la Iraq. Kwa mujibu wa ubalozi huo, Marekani na Iraq zililgharimia kwa pamoja bei ya meli hizo dola milioni 115.5, pamoja na vifaa vingine na mafunzo. Jeshi la Marekani lilikamilisha shughuli ya kuondoka Iraq mwezi Desemba 18 mwaka jana. Chini ya maafisa 200 wa jeshi la Marekani bado wako Iraq chini ya mamlaka ya ubalozi wa Marekani, ambapo wanasaidia katika usambazaji wa vifaa vya kijeshi na kuwapa mafunzo wanajeshi wa Iraq.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO