Tuesday, December 25, 2012

MKUU WA UJASUSI AUWAWA SYRIA

Waasi wa Syria wamemvamia,na kumuuwa afisa mmoja wa ujasusi wa kijeshi karibu na Damascus wakati jeshi la nchi hiyo likiendelea kushambulia ngome zinazoshikiliwa na waasi.Shirika la kuangalia haki za binaadamu nchini Syria limesema wapiganaji waasi walimvamia mkuu wa ujasusi wa kijeshi huko Jaramana jana usiku ambapo baadae aliuwawa.Jaramana ilioko kusini mashariki ya Damascus inakaliwa na Wakristo wengi na Wadruze na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.Mji huo umekuwa ukishambuliwa na mfululizo wa mabomu ya waasi katika miezi ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO