Afisa wa kike wa polisi nchini Afghanistan amempiga risasi na kumuua mshauri wa polisi wa Marekani ndani ya eneo la makao makuu ya polisi ya mji wa Kabul. Msemaji wa vikosi vya jumuiya ya kujihami ya NATO, amethibitisha tukio hilo, ambalo ni la kwanza kufanywa na afisa wa kike wa vikosi vya usalama dhidi ya wanajeshi wa kigeni. Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa Afghanistan, Mohammad Zahir, amalielezea tukio hilo kuwa ni shambulio la ndani, ambapo wanajeshi wa Afghanistan wanawashambulia wanajeshi wa kigeni, wanaopaswa kufanya nao kazi. Maafisa wasiopungua 52 wa NATO wameuawa mwaka huu na Wafghanistan waliovaa sare za polisi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO