Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa, utawala huo umeanza awamu mpya ya kupambana na wimbi la wahajiri wa Kiafrika wanaoingia huko Israel, kwa kuwarudisha kwenye nchi zao walizotoka. Netanyahu amesema kuwa, utawala huo pia unaweka mikakati ya kuweka doria ya kuzuia uingiaji kiholela wahajiri katika mpaka wenye urefu wa kilomita 240 kati ya utawala huo ghasibu na Palestina na Misri. Taarifa zinasema kuwa, wengi kati ya wahajiri hao ni raia kutoka Sudan na Eritrea na ambao hawako tayari kurejea kwenye nchi zao wakihofia kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka. Wahajiri hao mara kadhaa wamefanya maandamano wakitaka kukomeshwa vitendo vya unyanyasaji, ukandamizaji na vile vya kibaguzi vya utawala huo. Netanyahu aliwahi kusikika akisema kuwa, kuwepo Waafrika huko Israel ni pigo kubwa kwa utambulisho wa Uyahudi. Waafrika wanaoishi Israel wanakabiliwa na wakati mgumu, licha ya kuchomwa visu mara kwa mara na kuteketezwa moto makazi yao, hukumbana na vitendo kadhaa vya kibaguzi na hivi karibuni gazeti la Haaretz la Israel liliandika kuwa, chuki ya Waisraeli dhidi ya Waafrika na Waarabu inahamia kutoka kizazi hadi kizazi kingine huko Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO