Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa hivi karibuni itatuma wanajeshi 140 nchini Somalia chini ya mwamvuli wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM. Kayode Aderanti Afisa Mwandamizi wa Vikosi vya Kulinda Amani katika jeshi la Nigeria amesema kuwa, wanajeshi hao wa Nigeria wanatumwa nchini Somalia kutokana na makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya serikali ya Abuja na Umoja wa Afrika. Nchi ya Somalia inashuhudia mapigano na machafuko tokea ulipopinduliwa utawala wa Jenerali Muhammad Siad Barre mwaka 1991, kati ya serikali ya mpito na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka likiwemo al Shabab. Umoja wa Afrika tokea mwaka 2007 uliunda kikosi cha kulinda amani AMISOM kwa shabaha ya kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia kukabiliana na makundi ya waasi nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO