Monday, May 06, 2013

SITA WAKAMATWA SHAMBULIO LA ARUSHA


Polisi Mkoani Arusha nchini Tanzania inawashikilia watu 6 kwa madai ya kuhusika na mlipuko wa jana Jumapili katika Kanisa Katoliki la Olasit viungani mwa mji wa Arusha.nMiongoni mwa washukiwa hao ambao wako mikononi mwa polisi ni raia 4 wa Saudi Arabia, na wengine wawili  ni raia wa Tanzania.
Polisi mjini Arusha vilevile imethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio hilo la kigaidi ni wawili na kwamba wanachunguza ni mada za aina gani zilitumika wakati wa shambulizi hilo. Watu wengine 66 walijeruhiwa kwenye mlipuko huo. 
Hadi sasa hakuna taarifa zozote kuhusiana na chanzo halisi cha bomu hilo na hakuna kundi lililotangaza kuhusika na mlipuko huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO