Umoja wa Ulaya (EU) huenda ukauwekea vikwazo utawala haramu wa Israel kutokana na hatua yake ya kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika ardhi za Wapalestina unazozikalia kwa mabavu. Gazeti la kila siku la Maariv linalochapishwa Tel Aviv limeandika ripoti inayosema kuwa, EU inapanga kupiga marufuku bidhaa za Israel katika nchi za Ulaya pamoja na kutazama upya mkataba wa kibiashara kati ya utawala huo ghasibu na Umoja wa Ulaya. Hii ni katika hali ambayo, EU ilimuita balozi wa Israel kulalamikia rasmi hatua ya Tel Aviv ya kutangaza mipango ya kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika miji ya Quds Mashariki na eneo la Magharibi mwa Mto Jordan.
Friday, December 07, 2012
EU KUIWEKEA VIKWAZO ISRAEL KUFUATIA UPANUZI WAKE
Umoja wa Ulaya (EU) huenda ukauwekea vikwazo utawala haramu wa Israel kutokana na hatua yake ya kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika ardhi za Wapalestina unazozikalia kwa mabavu. Gazeti la kila siku la Maariv linalochapishwa Tel Aviv limeandika ripoti inayosema kuwa, EU inapanga kupiga marufuku bidhaa za Israel katika nchi za Ulaya pamoja na kutazama upya mkataba wa kibiashara kati ya utawala huo ghasibu na Umoja wa Ulaya. Hii ni katika hali ambayo, EU ilimuita balozi wa Israel kulalamikia rasmi hatua ya Tel Aviv ya kutangaza mipango ya kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika miji ya Quds Mashariki na eneo la Magharibi mwa Mto Jordan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO