Tuesday, December 18, 2012

RAIS WA IRAQ ALAZWA HOSPITALI

Rais Jalal Talabani , ambaye amekuwa mtu muhimu katika siasa za Iraq kwa miaka kadha na kuwa kama kiungo katika mgawanyiko wa madhehebu mbali mbali ya dini nchini humo ,alilazwa hospitali leo baada ya kuugua kwa ghafla. Talabani alifikishwa hospitali mjini Baghdad usiku wa jana. Hali hiyo imeeleza taarifa iliyowekwa katika tovuti ya rais kuwa imetokana na uchovu na kazi nyingi. Baadaye taarifa zilieleza kuwa viungo vyake vinafanyakazi vizuri na hali yake kiafya inaendelea vizuri. Mnadhimu mkuu wa Talabani, Nasser al-Ani , amekiambia kituo cha taifa cha televisheni kuwa rais alikuwa katika chumba maalum cha uangalizi wa wagonjwa mahututi katika hospitali ya Medical City mjini Baghdad lakini yuko katika hali nzuri.
Talabani amekuwa akisumbuliwa mara kwa mara na hali mbaya kiafya katika siku za hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO