Wednesday, December 19, 2012

IRAN YATAKA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA PAKISTAN KUZUIA MIHADARATI

Katibu Mkuu wa Tume ya Kupambana na Madawa ya Kulevya ya Iran ametaka kuimarishwa mashirikiano kati ya Iran na Pakistan katika fremu ya kupambana na mihadarati na kuzuia vitendo viovu na ugaidi katika mipaka ya nchi mbili hizo. Mustafa Muhammad Najar amesema kuwa kuimarishwa ushirikiano wa kiusalama kati ya Iran na Pakistan kupitia kubadilishana taarifa kwa wakati muafaka, kutasaidia kudhibitiwa vitendo viovu na pia kuwadhibiti magaidi kwenye mpaka wa pamoja wa nchi mbili hizo. Mustafa Muhammad Najar ameyasema hayo jana hapa Tehran mwishoni mwa kikao cha sita cha mawaziri wa pande tatu za Iran, Afghanistan na Pakistan katika mazungumzo kati yake na Naibu Waziri wa Pakistan anayehusika na mapambano dhidi ya mihadarati.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO