Tuesday, December 18, 2012

VIKWAZO VIMEONGEZA USTAWI WA IRAN

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kislamu ya Iran amesema kuwa vikwazo na vitisho vya maadui ni chanzo cha kushika kasi ustawi na maendeleo ya Iran ya Kiislamu. Akizungumza katika mkoa wa Mazandaran wa kaskazini mwa Iran, Rais Ahmadinejad amezishauri nchi za Magharibi kukomesha sera zao za uhasama dhidi ya taifa la Iran kwa sababu vikwazo ni kwa hasara ya nchi hizo.

Ahmadinejad amesema ustawi wa Iran umezitia wasi wasi nchi za Magharibi. Ameongeza kuwa wasi wasi huu umepelekea nchi hizo za Magharibi kuzidisha vikwazo na mashinikizo dhidi ya Iran. Rais Ahmadinejad amesema historia imethibitisha kuwa taifa la Iran ni la watu wastaarabu na kwamba utamaduni wa Iran daima umeibuka mshindi dhidi ya njama za kishetani za maadui na kubeba bendera ya tauhidi na uadilifu. Ahmadinejad amesema taifa la Iran daima linapenda uadilifu na uhuru kwa msingi wa usawa. Amesisitiza kuwa Iran daima imekuwa ikijieupusha na uhasana na inaamini kuwepo uhusiano na nchi zote kwa msingi wa kuheshimiana.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO