SAUDIA YAKASOLEWA HAKI ZA BINADAMU
Taasisi na asasi za kutetea haki za binadamu nchini Saudi Arabia zimetangaza kuwa, serikali ya Riyadh inawashikilia zaidi ya raia 600 wa mji wa Qatif, ulioko mashariki mwa Saudi Arabia katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Wakaazi wa mji huo wameeleza kuwa, viongozi wa Saudi Arabia wanatekeleza siasa za kibaguzi dhidi ya wakazi wa mji huo na hasa katika suala la ajira na haki za kiraia. Hali Kadalika wapinzani wa Saudi Arabia wamekuwa wakiitisha maandamano katika jimbo la al Qassim kwa shabaha ya kushinikiza kuachiliwa huru wanawake na watoto wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala wa Aal Saud. Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wametangaza kuwa, zaidi ya watu elfu sitini wanashikiliwa kwenye jela za nchi hiyo kwa tuhuma za kujishughulisha na masuala ya kisiasa. Wananchi wa Saudi Arabia kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita wamekuwa wakifanya maandamano ya amani yenye shabaha ya kutaka yafanyike mabadiliko ya mfumo wa kisiasa nchini humo, lakini wamekuwa wakikabiliwa na ukandamizaji unaofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO