TAHADHARI YA UN KUHUSU WAISLAM WA MYANMAR
Umoja wa Mataifa umetoa tahadhari kuhusiana na hali mbaya inayowakabili Waislamu wa jamii ya Rohingya wa nchini Myanmar. Martin Nesirky Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amebainisha kwamba, Waislamu wa Myanmar wanakabiliwa na hali mbaya sana na kwamba, kuna haja ya wananchi hao kufikishiwa misaada ya haraka. Wakati huo huo, mfuko wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, umetenga zaidi ya dola milioni tano kama bajeti ya misaada kwa Waislamu wakimbizi wa jimbo la Rakhine huko Myanmar ambao wanakadiriwa kufikia thelathini na sita elfu. Waislamu wa jamii ya Rohingya huko Myanmar wanaendelea kutendewa ukatili na Mabudha huku mashirika yanayodai kutetea haki za binaadamu ulimwenguni na madola ya Magharibi yakinyamaza kimya na kujifanya hayasikii kilio cha walimwengu cha kutaka kukomeshwa jinai dhidi ya Waislamu hao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO