Monday, December 03, 2012

SISITIZO LA HANIYA KUTEKELEZWA RIPOTI YA GOLDSTONE

Ismail Haniya Waziri Mkuu wa Serikali halali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina amesisitiza kuwa, utekelezwaji wa ripoti ya Jaji Richard Joseph Goldstone Mkuu wa Jopo la kutafuta ukweli la Umoja wa Mataifa kuhusiana na jinai za kivita zilizofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku 22 katika eneo la Ukanda wa Gaza, utazuia kukaririwa jinai za utawala huo ghasibu. Akizungumza na ujumbe wa Umoja wa Ulaya huko Gaza, Haniya ameongeza kuwa, iwapo ripoti ya Jaji Goldstone ingelitekelezwa ipasavyo na viongozi wa Kizayuni kukabidhiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC huko The Hague, utawala huo katu usingelithubutu kutenda jinai nyingine za kivita za siku nane huko Gaza. Jaji Richard Goldstone raia wa Afrika Kusini aliongoza jopo la kutafuta ukweli la Umoja wa Mataifa, kuchunguza tuhuma zilizowakabili viongozi wa Israel kwa kutenda jinai za kivita katika mashambulio ya siku 22 mwishoni mwaka 2008 hadi mwanzoni mwa mwaka 2009. Kwenye shambulio hilo, kwa akali Wapalestina 1,400 waliuawa shahidi na zaidi ya 5,000 kujeruhiwa. Inafaa kuashiria hapa kuwa, vita vya siku 8 vilivyoanzishwa na Wazayuni mwezi uliopita huko Gaza, vilipelekea Wapalestina 180 kuuawa shahidi na wengine 1,400 kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO