Monday, December 03, 2012

TAIFA HARAMU LA ISRAEL LAPINGA UAMUZI WA UN KUHUSU PALESTINA

Baraza la mawaziri nchini Israel limeukataa uamuzi wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa wa kuipa Palestina nafasi ya mwanachama mwangalizi wa Umoja huo asiye dola. Baraza hilo limesema kuwa hatua hiyo haitaundaa msingi wa majadiliano ya amani baina ya pande mbili zilizo kwenye mzozo. Uamuzi huo wa Israeli unakuja baada ya Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas kupata mapokezi ya kishujaa aliporejea mjini Ramallah akitokea Marekani alikoshuhudia mchakato wa kuipandisha hadhi Palestina. Abbas aliwaambia maelfu ya Wapalestina waliokusanyika kwenye Ikulu kuwa sasa wana taifa. Katika kupinga uamuzi huo wa umoja wa mataifa, Israel imesema kuwa kupandishwa hadhi kwa Palestina ndani ya umoja wa mataifa hakutaleta mabadiliko yoyote kwenye maeneo ya mzozo na kwamba hautawapora Wayahudi taifa lao wala haki zao za msingi. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewaambia mawaziri wake kuwa hatua hiyo ya umoja wa mataifa ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano uliosaini na serikali ya nchi hiyo. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO