Sudan imemnasa tumbusi au tai mzoga ambaye alikuwa anapaa angani akiwa na vifaa vya kijasusi vya utawala haramu wa Israel katika eneo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo.
Duru za usalama za Sudan zinasema tambusi huyo alikuwa na jukumu la kuufanyia ujasusi utawala haramu wa Israel. Katika mguu wa ndege huyo kulikuwa na plasitiki iliyofungwa yenye maandishi ya Kiibrania yaliyoandikwa "Huduma za Mazingira Israel" na " Chuo Kikuu cha Kiibrania, Jerusalem". Imedokezwa ndege huyo ana chombo cha kijasusi chenye uwezo wa kupiga picha na kuzipeleka Israel.
Hata hivyo Idara ya Mbunge za Wanyama Katika Utawala wa Kizayuni imedai kuwa ndege aliyekamatwa alikuwa na vifaa vya mawasiliano vinavyotumiwa na wataalamu kuchunguza ni sehemu zipi anazoruka.
Ikumbukwe kuwa Oktoba 24 Sudan ilisema ndege nne za Israel zilihujumu kiwanda cha silaha mjini Khartoum na kuwaua watu wanne. Mara kwa mara Sudan imekuwa ikiutuhumu utawala wa Israel kuwa unahusika katika kuchochea mapigano ya kikabila katika jimbo la Darfur.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO