Saturday, December 08, 2012

AFRIKA KUSINI YAMSAILI BALOZI WA ISRAEL KUHUSU UJENZI WAO

Afrika Kusini imemuita kumsaili Balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Pretoria juu ya mpango uliotangazwa na Tel Aviv wa kujenga maelfu ya nyumba zaidi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Ebrahim Ebrahim Naibu Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Afrika Kusini amesema, wamefanya hivyo ili kuonyesha jinsi wanavyotiwa wasiwasi na mpango huo wa ujenzi wa vitongoji vipya katika ardhi za Palestina. Israel ilitangaza mpango wake huo wa kujenga nyumba 3,000 na kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Quds Mashariki na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tarehe 30 Novemba. Hatua hiyo ilipasishwa ikiwa ni baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupasisha Palestina kuwa nchi mtazamaji asiye mwanachama katika umoja huo. Hatua hiyo ya kujipanua ya Israel imelalamikiwa na kupingwa duniani kote hata na washirika wake wa Umoja wa Ulaya. Pia Wapalestina wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka za kuizuia Israel kutojipanua zaidi na kupora ardhi za Palestina ambazo tayari inazikalia kwa mabavu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO