Maafisa kutoka Marekani na shirika la kujihami la NATO
wanasema jeshi la Syria limekuwa likifyatua makombora ya masafa mafupi katika
vita dhidi ya waasi, huku mzozo nchini humo ukizidi kuzorota.
Maafisa hao, ambao hawakutaka kutajwa, wanasema makombora
hayo, yanofanana na yale ya Scud, yalifyatuliwa kutoka Damascus hadi maeneo ya
kaskazini yanayodhibitiwa na waasi. SiasaMsemaji mmoja wa Wizara ya Nchi za
Kigeni wa Marekani, Victoria Nuland, alisema serikali ya Syria inatumia silaha
hatari. Ingawaje alisema kuwa hatatoa "habari za kinaganaga kuhusu
makombora hayo", alithibitisha kwamba "hivi majuzi ufyatuliaji wa
makombora ulikuwa umeonekana". Bi Nuland alisema: "Vile serikali hiyo
inavyozidi kukata tamaa ndivyo tunavyoshuhudia kuongezeka kwa visa vya ukatili
na kutumika kwa silaha kali zaidi."
Msemaji wa White House Jay Carney alisema iwapo taarifa
kusuhu urushaji wa Scud ni za kweli basi "hili ndilo tukio la hivi
karibuni kutoka serikali inayokata tamaa, na ambayo imepuuza umuhimu wa maisha
ya binadamu na wa wananchi wake". Jumatano, zaidi ya nchi 100 chini ya
jina Marafiki wa Syria, zilikutana nchini Morocco na kukubali kutambua upinzani
wa National Coalition for Syrian Revolutionary and Opposition Force, kiwe chama
pekee kitakachowakilisha wananchi wa Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO