Kitu Cha Kwanza Kinachohesabiwa
Katika ‘Amali Za Mja Ni Swalah
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ
َقَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ
((إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ
صَلاتُهُ فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ
وَخَسِرَ فَإِنْ انْتَقَصَ مِنْ فَرِيضَتِهِ شَيْءٌ قَالَ الرَّبُّ عَزَّ وَجَلَّ
انْظُرُوا هَلْ لِعَبْدِي مِنْ تَطَوُّعٍ فَيُكَمَّلَ بِهَا مَا انْتَقَصَ مِنْ
الْفَرِيضَةِ ثُمَّ يَكُونُ سَائِرُ عَمَلِهِ عَلَى ذَلِكَ)) الترمذي و أبوا داود
والنسائي وابن ماجه وأحمد
Imepokelewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kitu cha kwanza kinachohesabiwa
katika ‘amali za mja wa Allaah Siku ya Qiyaamah ni Swalah zake. Zikiwa
zimetimia, hapo tena atakuwa kaneemeka na kafuzu, na zikiwa zina kasoro atakuwa
kaanguka na kala khasara. Ikiwa pana upungufu katika Swalah zake za fardhi
Allaah ‘Azza wa Jalla Atasema: “Tazama ikiwa mja wangu ana Swalah zozote za
Sunnah ambazo zinaweza kufidia zile zilizopungua, hapo tena ‘amali yake
iliyobaki itaangaliwa hivyo hivyo)). [At-Tirmidhiy,
Abu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ahmad]
Maswali ya kujiuliza kuhusu Swalah:
1.Unaswali?
2.Unaziswali Swalah zote kwa wakati wake?
3.Unaziswali kwa twahara iliyokamilika na wudhuu uliotekelezeka
vizuri?
4.Unaelekea Qiblah? Unaweka Sutrah mbele yako?
5.Nguo na sehemu
unazoswalia ni safi hakuna najisi yoyote wala si isbaal; hazibururi kwa kuvuka mafundo
ya miguu?
6.Unaswali mahali au nyumba isiyotundikwa picha za viumbe?
7.Unaswali Jamaa’ah Msikitini? (Swalah kwa wanaume).
8.Unaswali kwa kutimizia kila kitendo cha Swalah ipasavyo?
9.Unasoma Qur-aan kwa kuzingatia maana yake?
10.Unaswali kwa khushuu’ (unyenyekevu) na twumaaninah (utulivu)?
11.Unaswali Swalah za Nawaafil na Sunnah; Sunnah zilosisitizwa na
zisositizwa, dhwuhaa, witr, tahajjud?
12.Je, unaziswalia nyumbani au umeiacha nyumba kugeuka kama kaburi?
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO