Sunday, December 23, 2012

TAMKO LA WAHADHIRI WA TANZANIA


TAMKO RASMI LA WAHADHIRI WOTE NCHINI TANZANIA
YAFUATAYO NI MATAMKO YA WAHADHIRI WA KIISLAMU WALIOKUTANA MJINI MOROGORO TAREHE 08/12/2012

WAHADHIRI WOTE KWA PAMOJA TUNASEMA:
1. HATUTAMBUI KUWEPO KWA UONGOZI MPYA WA WAHADHIRI.
2. TUNAMTAMBUA KONDO BUNGO KUWA NDIYO AMIRI WA WAHADHIRI NCHINI TANZANIA
3. TUNAITAMBUA SHURA YA MAIMAMU NA TUTASHIRIKIANA NAYO.
4. TUNATAMBUA NA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA NA TAASISI ZOTE ZA KIISLAMU
     TANZANIA.
5. TUNASEMA TAASISI ZOTE ZA KIISLAMU ZIMTAMBUE KONDO BUNGO BADO NI AMIRI
     WA WAHADHIRI.
6. KIKAO CHOCHOTE CHA WAHADHIRI KIITISHWE NA AMIRI KONDO BUNGO.
7. TUMEKUBALIANA KUTOWAUNGA MKONO NA KUTOWAPA USHIRIKIANO WALE
     WOTE WALIODHULUMU NA KUCHAFUA HARAKATI ZA DAAWA
8. WAHADHIRI WOTE WA MIKOANI KUTOA KAULI KWA VIONGOZI WA MISIKITINI
     KUTOSHIRIKIANA NA WALE WOTE WALIOJIPA MADARAKA KINYUME NA TARATIBU.
9. TUNALAANI KITENDO CHA SHEKHE PONDA NA WENZAKE KUNYIMWA DHAMANA  
    HALI KATIKA NCHI HII YA TANZANIA KUNA MTU KAUWA NA KAPEWA DHAMANA.
10.NCHI NZIMA IWATAMBUE WALE WOTE WALIOJIPA MADARAKA NI WAPINGA
      HARAKATI ZA DINI.
11.JUU YA UONGOZI MPYA YAFUATAYO
         i. KIKAO KILICHOFANYIKA CHA KUCHAGUA UONGOZI SIYO HALALI
         ii. KIKAO HAKIKUITISHWA NA AMIRI WA WAHADHIRI TANZANIA
        iii. WAHADHIRI WA MIKOANI HAWAKUSHIRIKISHWA
        iv. WAHADHIRI WA TANZANIA HATUNA TAARIFA YA KUJIUZULU KWA AMIRI WA    
            WAHADHIRI.
        v. MWEKAHAZINA WAO NDIO CHANZO CHA SHEKHE PONDA KUWA NDANI
           (MAHABUSU)
       vi. SHERIA YA UCHAGUZI HUO HAIKUTUMIKA KIUADILIFU
       vii. UONGOZI HUO HAUNA LENGO LA KUJENGA ILA UNALENGO LA KUWAGAWA
            WAISLAMU.
      viii. UMOJA HUO HAUKO PAMOJA NA VIONGOZI WALIOKAMATWA NA
            WANAOTAFUTWA.

12.TUNALAANI SANA KITENDO CHA BAADHI YA WAHADHIRI KUTUMIKA KWA AJILI YA MASLAHI YA MTU BINAFSI.
MWISHO WAHADHIRI WOTE KWA PAMOJA TUNAANDAA SIKU MAALUMU YA KUSOMA DUA YA PAMOJA KUWALAANI WOTE WALIOHUSIKA KUDHULUMU NA KUGAWA WAISLAMU
IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA KUTEULIWA WA HABARI ZA WAHADHIRI WA KIISLAMU TANZANIA
SHEIKH SULEIMAN NGUSURA

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO