Sunday, December 23, 2012

OIC: HALI YA KIBINADAMU UKANDA WA GAZA


Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imesema katika ripoti yake kwamba, hali ya kibinadamu huko Gaza Palestina ni mbaya. Taarifa ya OIC imebainisha kuwa, vituo vya afya katika Ukanda wa Gaza vinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawa na kwamba kwa uchache kuna aina 305 ya dawa ambazo hazipatikani kabisa katika vituo hivyo vya afya. Ripoti hiyo ya kila mwezi ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeashiria kuanza kwa msimu wa baridi na kusisitiza kwamba, kuna raia wengi wa Gaza ambao hawana makazi kwa sasa kutokana na nyumba zao kubomolewa kabisa katika vita vya siku nane vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, wananchi wa Ukanda wa Gaza wanaokabiliwa na mzingiro wa Israel wanakosa baadhi ya huduma muhimu anazozihitajia mwanadamu. Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu imezitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo pamoja na mashirika ya utoaji misaada ya kibinadamu kupelekea misaada ya haraka huko Gaza, Palestina kwa ajili ya kukabiliana na hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili wananchi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO