Thursday, December 20, 2012
UNCS WALAUMU UJENZI UNAOFANYWA NA ISRAEL
Wajumbe 16 wa Baraza la usalama la umoja wa Mataifa wametoa tamko la kuilaani Israel na mpango wake wa ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi Jerusalem ya mashariki. Marekani ndiyo nchi pekee ambayo haikulaani ujenzi huo unaotarajiwa kufanyika katika eneo lijulikanalo kama E1. Akizungumza mjini New york Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameitaka Israel kujizuia kutekeleza mpango huo ambao ameuelezea kuwa ni wa hatari kwa eneo la mshariki ya kati. Wanadiplomasia wanasema kuwa hatua hiyo ni matokeo ya kushindwa kwa mpango wa kuandikwa kwa azimio la kutafuta ufumbuzi wa suala hilo. Wakati huohuo taarifa zinasema kuwa Israel leo imepitisha mpango wa kujenga makaazi ya walowezi 500 ikiwa ni mwanzo wa mkakati wake wa kujenga nyumba 3000 kwenye eneo la Jerusalem mashariki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO