Thursday, December 20, 2012

RAIS MPYA WA KOREA AAHIDI MAHUSIANO MAZURI NA MAJIRANI WAO


Rais Mteule wa Korea ya Kusini Park Geun-Hye ameahidi kufanya juhudi katika kuimarisha mahusiano baina ya nchi hiyo na Korea Kaskazini wakati atakapochukua hatamu ya uongozi mwezi Februari mwakani. Katika hotuba yake ya kwanza ya kutangaza sera zake tangu alipotangazwa mshindi wa uchaguzi hapo jana, Bibi Park amesema kuwa atashirikiana na viongozi wenziwe wa eneo la Asia ya mashariki kutafuta maridhiano makubwa, ushirkiano na amani. Hata hivyo kiongozi huyo ameonya kuwa kitendo cha hivi karibuni cha Korea Kaskazini kurusha roketi angani kimeonyesha kuwa bado nchi hiyo ni kitisho kikubwa cha amani kwenye eneo hilo. Pamoja na ushirikiano, Park atalipa kipaumbele pia suala la usalama wa taifa lake. Kiongozi huyo ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kushika nafasi ya urais nchini Korea ya Kusini baada ya kupata wingi wa kura wa asilimia 51.6. dhidi ya Mpinzani wake Moon Jae alipata asilimia 47.6.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO