Friday, December 21, 2012

IRAN YAPINGA AZIMIO LA BARAZA KUU LA UN


Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa azimio la Baraza Kuu la Umoja huo dhidi ya Iran limepasishwa kwa malengo ya kisiasa na linapingana na ukweli wa mambo nchini Iran.
Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Muhammad Khazai amekosoa mbinu za kilaghai za kutumiwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa malengo ya kisiasa wakati wa kupigiwa kura azimio hilo na kusema kuwa haliakisi ukweli wa mambo nchini Iran.
Khazai amezikosoa pia Marekani na Canada ambazo ndizo zilizotayarisha rasimu ya azimio hilo kwa kudumisha siasa za kihasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa Tehran haitapiga magoti au kulegeza misimamo yake mbele ya mashinikizo hayo.
Alkhamisi ya jana Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio linalolaani kile kilichotajwa kuwa ni ukuikaji wa haki za binadamu nchini Iran. Azimio hilo limelaani adhabu ya kifo inazotolewa hapa nchini dhidi ya wahalifu na magenge ya magendo ya dawa za kulevya na kutaja adhabu hizo kuwa ni ukiukaji wa haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO