Friday, December 21, 2012

RUSSIA YAIKOSOA MAREKANI JUU YA HALI ZA KIBINADAMU

Rais wa Russia Vladimir Putin amekosoa vikali uvunjwaji wa haki za binaadamu nchini Marekani. Putin amekosoa vikali sheria ya kiuadui dhidi ya nchi yake inayofahamika kwa jina la Magnetiski ambayo imepitishwa hivi karibuni nchini Marekani na kuongeza kuwa, hatua hiyo ya Washington imeacha taathira hasi kwa mahusiano ya pande mbili. Putin ameyasema hayo katika kikao na waandishi wa habari, kilichohudhuriwa na waandishi wa habari wapatao 1600 na kukosoa mwenendo mbaya wanaofanyiwa watoto wa Kirusi ambao wamekuwa wakichukuliwa na raia wa Marekani na kufanywa kuwa watoto wao. Amesema watoto hao wa Russia wamekuwa wakifanyiwa ukandamizaji sambamba na kufikishwa katika mahakama za Marekani bila kuhudhuriwa kesi zao na waangalizi wa Kirusi. Amesisitiza kuwa, maafisa wa upelelezi wa Marekani wanawatesa kwa adhabu kali wafungwa mbalimbali katika gereza la Guantanamo bila ya kuwapatia haki zao za msingi. Rais wa Russia amesema, kwa mara kadhaa viongozi wa Marekani wamekuwa wakisema kuwa, watalifunga gereza hilo lakini zimekuwa ni ahadi zisizo na ukweli wowote na kwamba, Marekani inawazuilia katika gereza zake mbalimbali duniani maelfu ya wafungwa wasio na hatia. Akizungumzia uchaguzi wa rais uliomalizika nchini Marekani hivi karibuni Putin amesema, Marekani iliwazuia waangalizi wa kimataifa kuhudhuria zoezi la upigaji kura na kwamba Washington ililikalia kimya suala hilo bila kuchukua hatua zozote.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO