Katika kuendelea wimbi jipya la machafuko huko Libya, jumla ya wafungwa 196 wametoroka katika jela huko kusini mwa nchi hiyo. Afisa mmoja wa serikali za mitaa katika mji wa Sabha umbali wa kilomita 800 kusini mwa Tripoli mji mkuu wa Libya amesema kuwa karibu wafungwa 196 wametoroka katika jela moja mjini humo.
Afisa huyo amesema kuwa wafungwa hao waliotoroka walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa yasiyo ya kisiasa na kueleza baadhi ya wafungwa hao wametiwa mbaroni na wengine wangali wanasakwa. Kutoroka kwa wafungwa hao wote huko Libya ni ishara ya kuendelea hali ya ukosefu wa amani Libya ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu ushindi wa wanamapinduzi wa nchi hiyo dhidi ya utawala wa Kanali Muammar Gaddafi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO