Friday, December 07, 2012

AJALI YA NDEGE AFRIKA KUSINI 11 WAFARIKI

Habari kutoka Afrika Kusini zinasema kuwa watu 11 wamefariki dunia kufuatia ajali ya helikopta ya kijeshi katika maeneo yenye milima, mashariki mwa nchi hiyo. Duru za habari zinasema kuwa waliofariki dunia ni madaktari wa rais mustaafu, Nelson Mandela. Helikopta hiyo ilikuwa imetokea Pretoria ikielekea Mthatha karibu na mji wa Qunu, nyumbani kwa Mzee Nelson Mandela. Wakuu wa jeshi wanasema, shughuli za uokoaji zinaendelea ingawa hali mbaya ya hewa inafanya hali kuwa ngumu zaidi. Msemaji wa jeshi, Xolani Mabanga amesema atatoa taarifa kamili kuhusu ajali hiyo punde uchunguzi utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO