Maelfu ya Waisraeli wameandamana huko Tel Aviv wakilalamikia vitendo vya ukandamizaji, udhalilishaji na ubaguzi dhidi ya wanawake. Taarifa zinaeleza kuwa, maelfu ya Waisraeli hao waliandamana hapo jana wakati wa kukaribia maahdimisho ya siku ya kimataifa ya haki za binadamu. Sami Michael Mkuu wa Muungano wa Haki za Binadamu huko Israel amesema mbele ya waandamanaji hao kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel hutumia mabilioni ya dola kwa minajili ya kununua silaha na zana za kijeshi, amma hautengi bajeti kwa minajili ya kulinda haki haki za wanawake ambao kila siku wamekuwa wahanga wa kukandamizwa, kubaguliwa na hata kuuawa. Kabla ya hapo, maelfu ya Wazayuni waliandamana wakipinga sera za kiuchumi za Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO