Saturday, December 08, 2012

RUSSIA YATOA ONYO KUHUSU MAKOMBORA YA NATO UTURUKI

Russia imeonya kuwa Muungano wa Kijeshi wa NATO unaelekea kuingilia mgogoro wa Syria kufuatia hatua yake ya kuidhinisha kuweka makombora ya Patriot nchini Uturuki. Hayo yamesemwa na Alexander Grushko, balozi wa Russia katika makao makuu ya NATO mjini Brussels Ubelgiji. Ameongeza kuwa kuna tishio la NATO kujiingiza katika mgogoro wa Syria kutokana na madai ya kuwepo matukio ya kichokozi kutoka Syria. 

Uturuki imekaribisha hatua ya Muungano wa Kijeshi wa Nato ya kukubali kuweka makombora ya Patriot kwenye mpaka wa nchi hiyo na Syria. Hivi karibuni Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa NATO waliafiki ombi la serikali ya Ankara la kuweka aina hiyo ya makombora katika mpaka wake na Syria. Ngao hiyo ya makombora inatazamiwa kuwekwa huko kusini mwa Uturuki katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO