Sunday, December 02, 2012

WHITE HOUSE NA SENATE ZATOFAUTIANA KUHUSU IRAN


Ikulu ya White House nchini Marekani imeingia kwenye malumbano na Baraza la Senate kuhusu vikwazo vipya vilivyopitishwa siku chache zilizopita dhidi ya Iran. Taarifa ya White House imeelezea upinzani wake dhidi ya vikwazo hivyo na kusema athari zake zitaugusa pia uchumi wa Marekani. Ikulu ya white house imesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefika katika hatua ambayo, vikwazo vya kiuchumi pekee haviwezi kuipigisha magoti. 


Wabunge wa Marekani kwa kauli moja na katika hatua ya upande mmoja walipitisha duru mpya ya vikwazo dhidi ya sekta mbalimbali za kiuchumi za Iran. Viongozi wa Tehran wamesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari yoyote na badala yake vitakuwa mwiba wa kujichoma ambao hauambiwi pole.

 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO