Habari zinasema kuwa Marekani imeazimia kujenga kituo cha kijeshi cha chini ya ardhi kwa ajili ya utawala wa Kizayuni.
Gazeti la Washington Post limeandika kuwa timu ya wahandisi ya jeshi la Marekani imetangaza tenda ya makubaliano hayo ambapo kwa mujibu wake timu hiyo itajenga kituo cha kijeshi cha chini ya ardhi kitakachokuwa na ghorofa tano katika kituo cha jeshi la anga karibu na Tel Aviv. Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta ametangaza kuwa Washington itaendeleza misaada yake kwas Israel ili kuimarisha ngao za makombora ya utawala huo wa Kizayuni. Panetta amesema kuwa katika wiki chache zijazo Marekani inataraji kuipatia Israel mamilioni ya dola ili kuimarisha mfumo wake wa kujikinga na makombora.
Kuendelezwa uungaji mkono wa pande zote wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umekuwa na nafasi muhimu katika jinai za utawala huo kumekabiliwa na malalamiko na ukosoaji mkubwa kimataifa. Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza limeandika kuwa kundi la washindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na idadi kadhaa ya wasanii maarufu na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wametaka utawala wa Kizayuni uwekewe vikwazo vya kimataifa kutokana na mashambulizi yake ya kinyama ya hivi karibuni katika vita vya siku nane dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza.
Mairead Maguire, Nelson Mandela na Adolfo Perez Esquivel ni miongoni mwa wanaharakati watetezi wa amani na shakhsia wa kitamaduni na kisanaa waliosaini barua inayokosoa ushirikiano wa Marekani, Utawala wa Kizayuni na Umoja wa Ulaya na wametoa wito wa kuwekewa vikwazo utawala haramu wa Israel.
Hakuna shaka kuwa uungaji mkono wa hali na mali wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kwa utawala wa Kizayuni wa Israel umechangia sana katika kuendeleza jinai na vita vya utawala huo dhidi ya Wapalestina kama vile vita vya siku nane vya hivi karibuni huko Ghaza. Misaada rasmi ya Marekani isiyo na masharti ya kila ya mwaka kwa utawala wa Kizayuni ni dola bilioni tatu huku duru za kisiasa na za habari zikisema kuwa, misaada hiyo ya Marekani ni mikubwa zaidi kuliko kiwango hicho kilichotajwa. Imeelezwa kuwa Marekani inaipatia pia Israel misaada ya kijeshi isiyo na masharti kwa visingizo mbalimbali ambayo huwa haitangazwi.
Hii ni pamoja na kuwa Marekani na vilevile nchi za Ulaya huupatia utawala haramu wa Israel fedha na silaha za mabilioni ya dola ambazo sehemu yake kubwa hutumiwa na Israel kwa ajili ya kununulia silaha kutoka Marekani na nchi za Ulaya.
Kuongezeka misaada ya kijeshi ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni kunajiri katika hali ambayo katika miezi ya hivi karibuni pande hizo mbili zilishadidisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwa ajili ya kuimarisha mashirikiano ya kijeshi ya madola hayo ya kibeberu. Katika fremu hiyo wiki kadhaa kabla ya kuanza vita vya siku nane vya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Ghaza, Marekani na utawala wa Kizayuni zilifanya mazoezi makubwa ya kijeshi ambayo wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliyatathmini kuwa ni ruhusu ya Washington kwa utawala wa Kizayuni ili kwa ajili ya vita vya Ghaza.
Hata hivyo kushindwa Marekani kufikia malengo yake huko Iraq na Afghanistan na pia kushindwa kwa fedheha utawala wa Kizayuni wa Israel hivi karibuni katika vita vya siku nane dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza ni dhihirisho tosha kuwa Washington na Tel Aviv haziwezi kufuadafu licha ya kumiliki silaha za kisasa na kushirikiana pakubwa kijeshi mbele ya irada za mataifa mengine.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO