Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewataka Waislamu
kote duniani kuungana na kuzima njama za maadui. Rais Ahmadinejad ameyasema hayo
leo, katika sherehe za kumalizika kwa mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu
ya vikosi vya majeshi ya nchi za Kiislamu, yaliyofanyika mjini hapa Tehran kwa
mnasaba wa kuwadia uzawa wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na wiki ya Umoja. Akizungumzia udharura wa kuimarishwa umoja kati ya Waislamu wote duniani Rais
Mahmoud Ahmadinejad amesema kuwa, kuibua migongano na mizozo kati ya Waislamu ni
mbinu zinazofanywa na maadui kwa ajili ya kuzusha mifarakano kati yao.
Amesema kuwa, maadui mara zote wamekuwa wakifanya njama za kuanzisha mivutano
ya kikabila, kikaumu na kimadhehebu na kuongeza kuwa, pamoja na hayo Qur'ani na
Mtume Muhammad ni thamani za Waislamu wote duniani bali pia ni kwa ajili ya watu
wote wakiwemo wafuasi wa dini tofauti za mbinguni ikiwemo Uyahudi na Ukristo na
walimwengu wote kwa ujumla. Kwa upande mwingine Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema kuwa, moja ya sababu
zinazopelekea kuzushwa mivutano, ni kutokufahamu tafsiri halisi ya Qur'ani na
kwamba, suala hilo kwa muda mrefu limekuwa ndio chanzo cha matatizo kati ya
Waislamu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO