Kundi la waasi la Ansradeen la Mali lililokuwa limetangaza usitishaji vita wa upande mmoja mwezi Desemba uliopita, limetangaza kwamba, limefuta usitishaji vita huo. Taarifa ya kundi hilo la kaskazini mwa Mali imebainisha kwamba, limebadilisha msimamo wake wa kutaka kuhitimisha uhasama na serikali ya Bamako.
Taarifa zaidi kutoka Mali zinasema, wapiganaji wa kundi hilo sasa wanajiandaa tena kuanzisha mashambulio dhidi ya serikali. Aidha wapiganaji hao wamejiandaa kukabiliana na mashambulio ya kijeshi ya kimataifa. Itakumbukwa kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 20 mwezi uliopita lilipitisha azimio la kupelekwa askari wa kimataifa kaskazini mwa Mali, ili kukabiliana na makundi ya waasi. Aidha hivi karibuni Diango Cissoko Waziri Mkuu mpya wa Mali alitaka ufanyike haraka iwezekanavyo uingiliaji wa kijeshi wa nchi za Kiafrika kwa shabaha ya kukabiliana na makundi ya waasi huko kaskazini mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO