Friday, January 04, 2013

AUSTRALIA YAWAONYA RAIA WAKE

Raia wa Australia wanaoshiriki katika mapigano yanayoendelea nchini Syria wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha hadi miaka 20 gerezani.  Msemaji wa Waziri wa Mambo ya Kigeni, Bob Carr, ameyasema hayo leo baada ya raia mmoja wa nchi hiyo kuripotiwa kuuawa katika machafuko ya Syria. Msemaji huyo amesema serikali inafahamu kuhusu ripoti kwamba kuna zaidi ya WaAustralia 100 wanaoshiriki katika mapigano nchini Syria tangu mwaka wa 2011, lakini hana ushahidi wa raia wowote wanaohusika kwa sasa. Takriban raia watatu wa Australia wameripotiwa kuuawa nchini Syria, ikiwa ni pamoja na mtengenezaji matofali aliyedaiwa kutumia jina la Abu al-Walid al-Australi aliyeuawa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akipigana pamoja na waasi. Muasisi wa Baraza la Kiarabu la Australia, Joseph Wakim, amesema watu wengi wanaokwenda Syria wanadai kuwa wanatoa msaada wa kiutu kwa nchi hiyo inayokumbwa na vita lakini badala yake wanajiunga katika mapingano.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO