Umoja wa Afrika umeliomba Shirika la Kijeshi la NATO kujiunga na vikosi vyake huko Mali ili kusaidia kuwatokomeza waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo. Thomas Yayi Boni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amesema kuwa NATO inapaswa kutoa mchango wake huko Mali na kwamba kikosi cha Kiafrika kitaongoza njia kama ilivyofanywa na NATO huko Afghanistan.
Mwezi Disemba uliopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kutumwa wanajeshi huko Mali ili kuisaidia serikali ya nchi hiyo kupambana na waaasi wanaodhibiti eneo la kaskazini. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye nchi wanachama 15 lilipasisha kutumwa huko Mali kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa Kiafrika kwa muda wa mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO