Saturday, January 05, 2013

VYOMBO VYA USALAMA VY IRAN VYAONGOZA MASHARIKI YA KATI

Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imekiri kwamba vyombo vya usalama vya Iran ni miongoni mwa vyombo vyenye nguvu zaidi kati ya mashirika ya kijasusi duniani. Taarifa mpya iliyotolewa na Pentagon mwezi uliopita wa Disemba inaonyesha kuwa, vyombo vya usalama vya Iran vikiwa na wafanyakazi wapatao elfu thelathini vinahesabiwa kuwa ni vyenye nguvu kubwa zaidi kati ya mashirika ya kijasusi duniani kwani vimeweza kufanya operesheni kubwakubwa katika eneo la Mashariki ya Kati, Ulaya na hadi bara la Amerika. Taarifa hiyo yenye kurasa 64 inaeleza kuwa, Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imeweza kuingia kwenye maeneo yote yenye maslahi kwa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kujikusanyia taarifa na ripoti muhimu za kiusalama. Pentagon imeongeza kuwa, Iran ina kanali za kiintelijensia katika utawala wa Israel. Hivi karibuni Haydar Muslehi Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran alisema kuwa, Iran imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na njama zinazofanywa na vibaraka walio dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu zenye lengo la kuleta machafuko nchini. Amesisitiza kuwa, kikosi cha usalama wa taifa nchini kinadhibiti harakati zote za maadui hata zile ndogo kabisa zenye lengo la kuvuruga usalama wa taifa hapa nchini.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO