Saeed Jalili Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, mazungumzo kati ya Tehran na kundi la 5+1 yanatarajiwa kuanza hivi karibuni. Jalili ambaye ni kiongozi wa timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia na kundi la 5+1 linaloundwa na nchi 5 wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani amesema kuwa, mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika muda si mrefu.
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ambaye kwa sasa yuko mjini New Delhi India kwa safari ya kikazi amebainisha kwamba, hata hivyo hadi hasa pande husika hazijafikia makubaliano kuhusiana na tarehe hasa na mahala itakapofanyika duru ijayo ya mazunguzo ya nyuklia ya Iran na 5+1. Saeed Jalili amesisitiza kuwa, kama ambavyo Iran inafungamana kikamilifu na sheria za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, vivyo hivyo haiko tayari kufumbia macho haki yake ya kunufaika na nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani. Mara baada ya Jalili kukamilisha safari yake nchini India anatarajiwa kuelekea nchini Afghanistan.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO