Idadi ya vifo kutokana na bomu la kutegwa ndani ya lori ambalo liliwalenga mahujaji baada ya kumalizika ibada ya kila mwaka ya maombolezi ya kiongozi anayeheshihimiwa sana kwa waislamu wa madhehebu ya Shia imeongezeka hadi 23. Watu wengine 49 wamejeruhiwa katika mripuko huo wa jana jioni uliotokea katika mji wa Musayyib, ambao uko katika eneo linalouunganisha mji mkuu Baghdad na mji wa Karbala ambako mamilioni ya waumini wamekuwa wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya Arbadeen katika miaka ya karibuni. Miongoni mwa waliouawa ni wanawake na watoto. Mabomu mawili ya kutegwa kando ya barabara mashariki ya Baghdad, moja lililoripuka leo asubuhi, na jingine jana jioni, yamewajeruhi mahujaji16 wa Kishiya. Hakuna kundi lililodai haraka kuhusika na miripuko hiyo, lakini wanamgambo wa madhehebu ya Sunni kila mara hujaribu kuwalenga Washia wakati wa sherehe hizo za kila mwaka kwa lengo la kuzusha machafuko ya kimadhehebu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO