Monday, January 21, 2013

ISRAEL YAWATIMUA WATETEZI WA WAPALESTINA


Wanajeshi wa Israel wamelifukuza kundi la watetezi wa haki za Wapalestina kutoka kwenye kituo kilichopo kwenye Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kaskazini magharibi mwa Jerusalem. Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa Wapalestina 15 na wanaharakati wengine wa kigeni walikuwa wamejenga mahema manne mahali hapo, wakipinga ujenzi wa makazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi.
Msemaji huyo amesema kuwa jeshi liliwarifu wanaharakati hao juu ya hatua itakayochukuliwa dhidi yao, na kuwazuia wengine kwenda kwenye kambi hiyo. Wanajeshi wa Israel wameweka kizuizi cha barabarani karibu na kambi hiyo na walitumia mabomu ya kutoa machozi katika makabiliano na wanaharakati hao. Tarehe 13 mwezi huu wa Januari, Israel ilikihamisha kituo kikubwa katika eneo linalozozaniwa kati ya Jerusalem ya Mashariki na makaazi ya walowezi ya Ma'aleh Adumin.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO