Idadi ya mateka waliouawa katika kisa cha utekaji nyara kwenye mtambo wa gesi nchini Algeria imepanda na kufika watu 60, huku kukiwa na taarifa kuwa miongoni mwao ni raia tisa wa Japan. Waziri Mkuu wa Algeria, Abdelmalek Sellal, anatarajiwa kutoa maelezo zaidi katika mkutano na waandishi wa habari baadaye leo, juu ya kisa hicho cha utekaji nyara ambacho ni mojawapo ya vibaya zaidi kutokea katika kipindi cha muongo mmoja.
Raia wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Norway, Japan, Norway na Romania waliuawa na wengine hawajulikani walipo. Chanzo kutoka vyombo vya usalama vya Algeria kimesema kuwa wanajeshi waligundua maiti nyingine 25 jana, na kuifanya idadi ya mateka waliouliwa kufika 48, na idadi kamili ya vifo katika mkasa huo kufikia 80.
Taarifa zaidi zinasema kwamba miongoni mwa wanamgambo wa Kiislamu waliouawa kwenye tukio hilo ni raia wawili wa Canada wenye asili ya Algeria. Mokhtar Belmokhtar, anayetambuliwa kama mmoja wa viongozi wa al-Qaida, amedai kupanga utekaji nyara huo. Wanamgambo wa Kiislamu waliuvamia mtambo huo wa gesi kama ulipaji kisasi kwa operesheni za kijeshi za Ufaransa nchini Mali.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO